CHELSEA WAFIKIA MAKUBALIANO YA KUMSAJILI PEP CHAVARRÍA
Chelsea imefikia makubaliano na Rayo Vallecano ya kumsajili beki wa kushoto wa Uhispania Pep Chavarría kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Klabu hiyo ya London italipa euro milioni 19 pamoja na nyongeza ya hadi euro milioni 2 kulingana na masharti ya mkataba, huku mchezaji huyo akitarajiwa kusafiri kwa ajili ya vipimo vya afya na kusaini mkataba wake.
Hatua ya mwisho ya kukamilisha uhamisho huo ni kusainiwa kwa nyaraka rasmi kati ya klabu hizo mbili kabla ya Chavarría kutambulishwa rasmi kama mchezaji mpya wa Chelsea.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































