#Football #Sports

INGWEE YAILEMEA PAMBA JIJI YA TANZANIA HUKU IKIENDELEA KUJINOA KUELEKEA MSIMU MPYA

AFC Leopards imeongeza maandalizi yake kuelekea msimu wa 2026/27 kwa kupeleka kikosi chake nchini Tanzania kwa mechi za kirafiki. Kocha Fred Ambani anatumia mechi hizo kuwaandaa wachezaji kabla ya msimu mpya kuanza.

Timu hiyo yenye mataji 12 ya ligi ya Kenya ilicheza na Pamba Jiji FC ya Tanzania mjini Mwanza Jumamosi na kuilemea kwa bao moja sufuri bao lilofungwa na James Kinyanjui. Leopards leo inatarajiwa kukutana na Kagera Sugar katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Kocha Ambani anatumia mechi hizi kuwapima wachezaji wake na kuimarisha kikosi. Mechi hizo pia zitampa nafasi ya kujaribu mbinu na mipangilio tofauti kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *