#Local News

SERIKALI IMETENGA SHILINGI MILIONI 281.2 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI

Serikali kupitia Shirika la TANATHI imetenga shilingi milioni 281.2 kwa ajili ya kutekeleza miradi 17 ya maji katika kaunti za Makueni, Kitui, Machakos na Kajiado.

Miradi hiyo inatarajiwa kukamilika kabla ya kuanza kwa mvua za El Niño, ili kusaidia wakazi wa maeneo hayo kuhifadhi maji kwa matumizi ya baadaye.

Serikali imesema miradi hiyo inalenga kuimarisha upatikanaji wa maji na kupunguza changamoto ya uhaba wa maji kwa wananchi katika maeneo hayo.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

SERIKALI IMETENGA SHILINGI MILIONI 281.2 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI

DKT PETER MBAE WA DCP AMESEMA UPINZANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *