BOINETT: SERIKALI INALINDA KENYA DHIDI YA VITISHO VYA USALAMA
Mshauri wa Usalama wa Taifa Joseph Boinett amesema vitisho vya usalama vina sura mbalimbali na jukumu la serikali ni kuwalinda Wakenya dhidi ya hatari zinazotoka ndani na nje ya mipaka ya nchi.
Boinett amesema serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na vitisho hivyo, akisisitiza kuwa usalama wa taifa ni jukumu muhimu katika kulinda maisha na mali ya wananchi.
Amesema juhudi hizo zimechangia Kenya kubaki na utulivu na amani licha ya changamoto za kiusalama zinazokumba baadhi ya mataifa katika eneo hili la Afrika Mashariki.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































