KAMATI YA ULINZI YA BUNGE YAPOKEA MALALAMISHI DHIDI YA WANAJESHI WA UINGEREZA (BATUK)
Madai ya mwanajeshi wa uigereza wanaofanya mazoezi humu nchini ya kumuua Agness Wanjiru 2012 yamepelekea familia yake kuilaumu idara ya upelelezi DCI na afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma ODPP kwa kutatiza mchakato wa kupata haki.
Akiwa mbele ya kamati ya bunge la kitaifa ya ulinzi msemaji wa familia hiyo Esther Muchiri amezishutumu idara hizo akidai kwamba zimekuwa zikishirikiana na serikali ya uingereza kumficha afisa alihusika na kifo cha mpendwa wao.
Familia sasa inaitaka kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa belgot nelson Koech kuwasaidia kupata haki.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































