#Business

MAREKANI YAMEZEA MATE MADINI YA KENYA 

Marekani imeongeza hamu yake katika madini muhimu ya Kenya wakati ambapo serikali ya Rais William Ruto inataka kuendeleza uwezo wa kuchakata madini ndani ya nchi badala ya kuyauza nje yakiwa ghafi.

Suala hilo limejitokeza kwa uzito wakati wa mkutano kati ya Rais Ruto na Waziri wa Masuala ya Kigeni  wa Amerika, Marco Rubio, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) jijini New York.

Kwa mujibu wa taarifa Wizara ya Masuala ya Kigeni ya Amerika, viongozi hao wawili wamejadili diplomasia ya biashara pamoja na amani na usalama wa kikanda, huku madini muhimu yakitajwa kama eneo kuu la ushirikiano wa kiuchumi. Waziri huyo ametafutia kampuni za Amerika nafasi ya kushiriki katika sekta hiyo.

Imeatayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *