SAKA: ENGLAND BADO INA MAJERAHA BAADA YA KUFELI KOMBE LA DUNIA
Winga wa Arsenal Bukayo Saka amesema kikosi cha Uingereza bado kina maumivu ya kushindwa katika nusu fainali ya Kombe la Dunia, licha ya kumaliza mashindano hayo katika nafasi ya tatu.
Uingereza inaanza kampeni yake ya Ligi ya Mataifa dhidi ya mabingwa wa dunia Hispania katika Uwanja wa Wembley Septemba 26, wiki tisa baada ya kufungwa mabao mawili ya dakika za mwisho na Argentina katika nusu fainali ya Kombe la Dunia.
Saka alifunga mabao matatu Uingereza ilipoishinda Ufaransa 6-4 na kumaliza ya tatu, lakini amesema uchungu wa kushindwa kutwaa taji lao la kwanza kubwa tangu Kombe la Dunia la 1966 bado unaendelea.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































