UHURU ADAI RAILA ALISHINDA UCHAGUZI WA 2022
Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amedai kuwa aliyekuwa kiongozi wa ODM Raila Odinga alishinda uchaguzi wa urais wa 2022 lakini akanyimwa ushindi kupitia kile alichokiita hila za uchaguzi.
Akizungumza katika mkutano wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya Chama cha Jubilee jijini Nairobi, Uhuru amesema alimuunga mkono Raila wakati wa kampeni ili kuhakikisha anashinda urais.
Kauli hiyo imekosolewa na Chama cha Muungano wa Kidemokrasia, UDA, kinachosisitiza kuwa Rais William Ruto alishinda uchaguzi huo kwa haki.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































