KABRAS SUGAR KUCHEZESHA CHIPUKIZI KAMPALA SEVENS
Kabras Sugar itatuma kikosi cha vijana katika Mashindano ya Raga ya Saba ya Kimataifa ya Kampala Oktoba 3 na 4, kocha Ntabeni Dukisa akithibitisha uamuzi huo.
Dukisa amesema uamuzi huo umetokana na wachezaji wa kikosi cha kwanza kuwa katika timu za Morans na Shujaa zinazojitayarisha kwa Kombe la Afrika la Raga ya Saba nchini Mauritius na mashindano ya Safari Sevens jijini Nairobi.
Amesema mashindano ya Kampala yatawapa wachezaji chipukizi wa klabu hiyo nafasi ya kujipima dhidi ya wapinzani wenye ubora na kupata uzoefu Zaidi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































