#Football #Sports

JUNIOR STARS YAPATA DJIBUTI NA TANZANIA KATIKA MCHUJO WA AFCON

Kenya imepangwa Kundi C pamoja na Djibouti na Tanzania katika michuano ya mchujo ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ya Kombe la Afrika kwa vijana chini ya miaka 17.

Mchujo huo utafanyika jijini Kigali Rwanda kuanzia Oktoba 10 hadi 19, huku timu itakayoongoza kila kundi ikifuzu hatua ya nusu fainali pamoja na timu bora iliyomaliza nafasi ya pili.

Timu mbili bora katika mchujo huo zitaiwakilisha kanda ya Afrika Mashariki na Kati katika Kombe la Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 mwaka 2027.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *