MAAFISA WA UPELELEZI WAOKOA WATU 17 WAETHIOPIA KUTOKANA NA ULANGUZI WA BINADAMU
Watu 17 wanaoaminika kuwa waadhiriwa wa ulanguzi wa binadamu wameokolewa na Makachero wa DCI wa kitengo cha kukabili uhalifu wa kimataifa.
Kwa mujibu wa maafisa hao wa DCI baada ya kupokea taarifa za kijasusi waliweka mitego katika daraja la makupa ambapo walifanikiwa kumkamata dereva na utingo wake pamoja na gari lililokuwa linatumika katika usafirishaji wa waadhiriwa hao.
Washukiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo hii.
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































