#Local News

GAVANA NATEMBEYA AMESEMA SIFUNA ATATUMIA UDP KUWANIA URAIS

Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya amesema Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna atatumia chama cha United Democratic Party, UDP, kuwania urais huku viongozi wa upinzani wakijadiliana kuhusu uwezekano wa kumpata mgombea mmoja wa urais.

Natembeya amesema vyama vya upinzani bado ni sehemu ya muungano mmoja licha ya baadhi ya viongozi kuendelea na mipango ya kuanzisha vyama vyao vya kisiasa.

Ametolea mfano Muungano wa Azimio ambao alisema ulihusisha takriban vyama 25 vilivyomuunga mkono aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *