#Local News

KENYA KWANZA: KAZI NDIO ITAKAYOAMUA UCHAGUZI WA 2027

Viongozi wanaounga mkono serikali ya mseto wamesema uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 hautaamuliwa kwa makelele ya kisiasa bali rekodi ya kazi na matokeo ambayo viongozi watawasilisha mbele ya Wakenya

Wakizungumza katika kaunti tatu tofauti, viongozi hao wamemlenga kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua, wakisema upinzani unaonekana kutumia kauli kali za kisiasa bila kuweka mezani ajenda mbadala yenye suluhu kwa changamoto zinazowakabili wananchi

Wamesema wakati wa kampeni za maneno pekee umefika ukingoni, na Wakenya wanapaswa kupima viongozi kwa kile walichotekeleza na mipango waliyonayo ya kuboresha maisha ya wananchi kabla ya kuamua hatima ya uchaguzi wa 2027.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *