#Local News

UASU IMEIPA SERIKALI NOTISI YA SIKU SABA YA MGOMO

Chama cha Wahadhiri wa Vyuo Vikuu, UASU, kimeipa serikali notisi ya siku saba ya mgomo kutokana na mkwamo wa makubaliano ya mkataba wa pamoja wa maslahi ya wafanyakazi, CBA, wa mwaka 2025 hadi 2029.

UASU imesema wahadhiri katika vyuo vikuu vyote vya umma wanatarajiwa kugoma kuanzia tarehe 2 Oktoba, hatua inayoweza kutatiza masomo wakati wanafunzi wa mwaka wa kwanza wakianza muhula wao wa kwanza wa mwaka wa masomo wa 2026.

Muungano huo umesema serikali imeshindwa kuwasilisha pendekezo la upande wake kuhusu CBA ya 2025 hadi 2029, licha ya mazungumzo kuhusu makubaliano hayo kuendelea.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *