KIPKORIR AWEKA LENGO LA MEDALI YA DUNIA 2027
Bingwa wa fainali ya mita 5,000 ya Ligi ya Diamond ya mwaka 2022 Nicholas Kipkorir sasa ameelekeza nguvu zake katika kulenga nafasi za juu kwenye mbio za mita 10,000 katika Mashindano ya Dunia ya Riadha ya mwaka 2027 mjini Beijing.
Kipkorir mwenye umri wa miaka 27 alishinda medali ya fedha katika Mashindano ya Dunia ya Mbio za Barabarani yaliyofanyika Copenhagen, Denmark, baada ya kumaliza mbio za nusu marathon kwa dakika 58 na sekunde 11, sekunde tano nyuma ya Andreas Almgren wa Sweden aliyeshinda dhahabu kwa 58:06.
Medali hiyo ya fedha imekuwa hatua kubwa kwa Kipkorir ikilinganishwa na mashindano ya mwaka 2023 mjini Riga, Latvia, ambako alishinda medali ya shaba katika mbio za barabarani za kilomita tano kwa muda wa dakika 13 na sekunde 16.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































