MUDAVADI ATOA WITO KWA NCHI KUONGOZA MICHAKATO YA AMANI
Mkuu wa Baraza la Mawaziri Musalia Mudavadi amezitaka nchi kumiliki na kuongoza michakato yao ya amani, akisema utulivu wa kudumu huimarika zaidi pale suluhu zinapoandaliwa na watu wanaoishi na changamoto hizo.
Akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa Mawaziri wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kujenga Amani mjini New York, Mudavadi amesema washirika wa kimataifa wanapaswa kuimarisha uongozi wa kitaifa na uwezo wa wenyeji pamoja na kuzingatia vipaumbele vya wananchi.
Mudavadi amesema msimamo wa Kenya ni kwamba taasisi imara na shirikishi ndizo msingi wa kujenga amani endelevu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































