KURIA AIBUA MADAI YA KUVURUGWA KWA UCHAGUZI WA 2013
Waziri wa zamani Moses Kuria amedai kuwa yeye pamoja na wanasiasa wengine walipanga mikakati ya kuvuruga uchaguzi wa urais wa mwaka 2013 ili kumpa ushindi aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta.
Akizungumza katika kituo Kimoja humu nchini, Kuria amesema walitumia mbinu za siri na kuanzisha kesi mahakamani kuhusu kura zilizokataliwa, huku akidai seva za IEBC ziliingiliwa ili kuzuia uchaguzi wa marudio wa urais.
Kuria amesema kesi hiyo kuhusu kuhesabiwa kwa kura zilizokataliwa ilisaidia kuhakikisha Kenyatta anashinda uchaguzi huo, akitoa madai hayo wakati mjadala kuhusu matokeo ya uchaguzi wa 2022 ukiendelea.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































