POLISI MOMBASA WAMEMKAMATA MWANAUME MMOJA KWA KUMUUWA MKEWE NA MTOTO
Polisi mjini Mombasa wanamshikilia mwanamume mmoja anayedaiwa kumuua mkewe na mmoja wa watoto wao kwa kuwachoma kisu, kufuatia mzozo wa kifamilia katika eneo la Shauri Yako Mkomani Nyali kaunti ya Mombasa.
Taarifa ya polisi kutoka Kituo cha Kongowea inamtaja mshukiwa huyo kama Richard Matiko, ambaye pia anadaiwa kumshambulia mtoto wao mwingine mwenye umri wa miaka 14 na kumsababishia majeraha makubwa.
Mtoto huyo alitoroka na baadaye kupelekwa katika Hospitali ya Coast General Teaching and Referral na msamaria mwema, ambapo anaendelea na matibabu.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































