RUTO AITAKA UN KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA
Rais William Ruto ametaka Umoja wa Mataifa kufanya mageuzi ya haraka akisema mfumo wa sasa wa uongozi duniani hauakisi hali na mahitaji ya dunia ya leo.
Akihutubia Mkutano Mkuu wa 81 wa Umoja wa Mataifa mjini New York, Ruto ametaka Afrika ipewe uwakilishi wa kudumu na wa usawa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Ruto pia ametoa wito wa kufanyiwa mageuzi mfumo wa fedha wa kimataifa ili kukidhi mahitaji ya mataifa katika mazingira ya sasa ya uchumi wa dunia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































