KALONZO AIBUA UPYA MADAI YA USHINDI WA RAILA KATIKA CHAGUZI
Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amedai aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga alinyang’anywa ushindi katika chaguzi za urais za 2013, 2017 na 2022, akifufua mjadala kuhusu matokeo ya chaguzi hizo.
Akizungumza Kaunti ya Kitui, Kalonzo ametetea madai ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuwa Raila alinyang’anywa ushindi wa 2022 na kuitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kuwahakikishia Wakenya uchaguzi huru na wa haki mwaka ujao.
Madai hayo yameibua tena mjadala wa kisiasa na kuzua majibu makali kutoka kwa baadhi ya viongozi, wakiwemo watu wa karibu na familia ya Raila Odinga.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































