#Local News

IGAD YAONYA EL NINO KUTISHIA CHAKULA NA MIFUGO AFRIKA MASHARIKI

Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali Afrika Mashariki IGAD imeonya kuwa mvua kali za El Nino zinatishia usalama wa chakula, mifugo na miundombinu katika eneo la Afrika Mashariki.

Akizungumza katika kongamano la maandalizi ya kukabiliana na majanga mjini Addis Ababa, Naibu Katibu Mkuu wa IGAD Mohamed Abdi Ware amesema nchi za ukanda huu zinapaswa kuchukua hatua mara moja badala ya kutegemea utabiri pekee.

Ware amesema hatua za mapema ni muhimu katika kuwalinda wananchi walio katika hatari pamoja na kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *