WANGA AMTAKA UHURU AACHE KUCHOCHEA WAKENYA KWA KAULI ZA 2022
Mjadala kuhusu matamshi ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kuhusu uchaguzi wa mwaka 2022 umeendelea kuchacha, huku Mwenyekiti wa Kitaifa wa ODM Gladys Wanga akimtaka kuacha kurejelea suala hilo kwa kile anachodai ni kuchochea hisia za Wakenya.
Akizungumza katika Kaunti ya Kajiado, Wanga amedai kuwa Uhuru alimhadaa marehemu Raila Odinga wakati wa mchakato wa uchaguzi huo, kauli iliyozua mjadala zaidi kuhusu yaliyotokea mwaka 2022.
Kauli nyingine kuhusu suala hilo zimetolewa na Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka pamoja na Kinara wa chama cha PM na Mbunge wa Saboti Caleb Amisi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































