#Local News

NAIBU INSPEKTA WA POLISI MASENGELI AMEWAONYA WANASIASA DHIDI YA MATAMSHI YA UCHOCHEZI

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli amewaonya wanasiasa dhidi ya kutumia matamshi ya chuki na uchochezi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

Masengeli amesema viongozi wanapaswa kuhamasisha amani na utangamano miongoni mwa Wakenya badala ya kutumia siasa kuchochea migawanyiko.

Amesisitiza kuwa vyombo vya usalama vitachukua hatua dhidi ya watu watakaokiuka sheria kwa kueneza matamshi ya chuki au kuchochea vurugu.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *