MURANG’A SEAL YAICHARAZA POSTA RANGERS 5-1
Murang’a Seal ilipata ushindi mkubwa zaidi msimu huu wa Ligi Kuu ya FKF baada ya kuicharaza Posta Rangers mabao 5-1 katika uwanja wa SportPesa Arena.
Majaliwa Charo na Josphat Lopaga walifunga mabao mawili kila mmoja, huku Michael Macharia akiongeza bao jingine katika mechi ya kwanza ya Murang’a nyumbani msimu huu.
Ushindi huo umeiwezesha Murang’a kujirekebisha baada ya kufungwa 4-2 na mabingwa watetezi Gor Mahia, huku Posta Rangers ikipata kichapo cha pili mfululizo baada ya kupoteza 1-0 dhidi ya Shabana FC.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































