ODHIAMBO ANG’ARA KATIKA MASHINDANO YA NGUMI
Bondia Mkenya Emmanuel Odhiambo, ambaye pia hufanya kazi ya bodaboda jijini Nairobi, ameibuka mshindi katika mashindano ya ngumi ya Afrika kwa mabondia wakubwa yanayoendelea Kasarani.
Odhiambo alimshinda Zienalabden Ismael wa Sudan katika uzani wa bantam, akitumia mbinu bora za kujihami, mwendo wa haraka na mashambulizi sahihi kupata ushindi wa majaji.
Ushindi huo unaimarisha matumaini ya timu ya Kenya, maarufu kama The Hit Squad, ya kutwaa medali nyingi katika mashindano hayo yanayoandaliwa nyumbani.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































