MVUTANO WA NYORO NA METHU WAYUMBISHA UPINZANI
Mivutano ndani ya upinzani imeongezeka baada ya kiongozi wa chama cha PPK Ndindi Nyoro na katibu mkuu wa DCP John Methu kurushiana tuhuma, hali inayotishia juhudi za kuunda umoja kabla ya uchaguzi wa 2027.
Nyoro, akiwa katika ziara ya kisiasa kaunti ya Kajiado pamoja na naibu kiongozi wa Jubilee Fred Matiang’i, amekanusha madai ya Methu kwamba yeye ni mpelelezi wa serikali ndani ya upinzani.
Nyoro naye amedai kuwa Methu huenda akawa ndiye anayeshirikiana na serikali kuvuruga upinzani, akitaja uhusiano wake wa karibu wa awali na Rais William Ruto.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































