KINDIKI AONYA WANAOCHOCHEA VURUGU ZA KISIASA
Naibu Rais Kithure Kindiki amewaonya wanasiasa dhidi ya kuchochea vurugu na kutumia makundi ya vijana kuvuruga amani, huku joto la kisiasa likizidi kupanda kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Giathenge–Witima eneo la Othaya, kaunti ya Nyeri, Kindiki amesema vyombo vya usalama vinawafuatilia wanasiasa wanaoshukiwa kuandaa makundi ya wahuni kabla ya kampeni kuanza.
Amewataka vijana kukataa kutumiwa kuchochea ghasia, huku akiwataka wapinzani wake wa kisiasa katika eneo hilo kushindana kwa sera na mipango ya maendeleo badala ya siasa za uharibifu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































