WANGA ASEMA UPINZANI HAUNA AJENDA
Baadhi ya viongozi wa ODM, wakiongozwa na mwenyekiti Gladys Wanga, wameushutumu upinzani kwa kukosa ajenda ya Wakenya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Wakizungumza kaunti ya Migori, viongozi hao wamewahimiza wananchi kumuunga mkono Rais William Ruto, wakisema ana nafasi ya kuwashinda wapinzani wake katika uchaguzi.
Waziri wa Utumishi wa Umma, Geoffrey Ruku, pia ameusuta upinzani kwa kupinga rekodi ya maendeleo ya serikali, akitaja miradi inayotekelezwa katika maeneo ya Nyanza na Magharibi mwa Kenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































