IEBC INAZINGATIA KUONGEZA VITUO VYA KUPIGIA KURA KWA WAKENYA WANAOISHI NJE YA NCHI
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC inazingatia kuongeza vituo vya kupigia kura kwa Wakenya wanaoishi nje ya nchi kutoka nchi 12 zilizohudumia uchaguzi mkuu wa 2022 hadi nchi 26 katika uchaguzi wa mwaka 2027.
Mpango huo ukitekelezwa utaongeza idadi ya nchi ambako Wakenya wanaoishi ughaibuni wataweza kujisajili na kushiriki katika uchaguzi chini ya mfumo wa upigaji kura wa diaspora wa tume hiyo.
Kwa mujibu wa mfumo huo, kila nchi inayoshiriki katika upigaji kura wa diaspora huhesabiwa kuwa kituo kimoja cha kupigia kura wakati wa kujumlisha kura, hata iwapo zoezi la upigaji kura litafanyika katika zaidi ya ubalozi mmoja wa Kenya nchini humo.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































