ARTETA ATAZIMIA KUTETEA TAJI LA LIGI
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema kina cha kikosi chake kitakuwa muhimu katika kutetea taji la Ligi Kuu ya England, baada ya Noni Madueke kutoka benchi na kufunga bao la ushindi wa 1-0 dhidi ya Nottingham Forest.
Arsenal ilikosa kiwango chake bora katika mechi hiyo iliyochezwa City Ground, na haikupiga shuti lolote lililolenga lango hadi Madueke alipofunga dakika ya 80.
Licha ya ushindi huo mwembamba, Arsenal imejipunguza hadi pointi tatu nyuma ya vinara Manchester City, ikiendeleza matumaini yake ya kutetea taji.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































