WATU WANNE WAKAMATWA KWENYE MAANDAMANO YA BEI YA MAFUTA
Watu wanne wamekamatwa jijini Nairobi wakati wa maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta na gharama ya maisha, yaliyofanyika siku ya Mashujaa.
Waandamanaji waliingia mitaani kutaka serikali ipunguze bei ya mafuta na kuchukua hatua za kupunguza makali ya maisha kwa wananchi.
Miongoni mwa waliokamatwa ni mwandishi wa habari wa Citizen TV, Francis Odee, aliyekuwa akiripoti maandamano hayo, huku maswali yakiibuka kuhusu uhuru wa wanahabari.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































