#Local News

KAMPENI YA MIEZI SITA YA KUANGAZIA UKATILI WA KIJINSIA YAANZISHWA

Kampeni ya miezi sita ya kuongeza uelewa kuhusu ukatili wa kijinsia imezinduliwa katika Kaunti ya Vihiga, huku visa vya ukatili huo vikiongezeka nchini.

Kampeni hiyo imezinduliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Jinsia Anne Wang’ombe, ikiwa na lengo la kuelimisha umma kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia na namna ya kukabiliana nao.

Uzinduzi huo unafanyika wakati ambapo wadau wanazidisha wito wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kukomesha ukatili wa kijinsia na kulinda waathiriwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *