#Local News

MOSIRIA ADOKEZA SABABU YA KUFUTWA KAZI

Aliyekuwa afisa mkuu wa kaunti ya Nairobi, Geoffrey Mosiria, amedokeza kuwa kufutwa kwake kazi na Gavana Johnson Sakaja kulitokana na kile alichokitaja kuwa kumzidi bosi wake kwa umaarufu.

Kuondoka kwa Mosiria kunafuatia mabadiliko makubwa katika baraza la mawaziri la kaunti yaliyotangazwa na katibu wa kaunti Machel Waikenda.

Hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada ya Mosiria kutangaza azma yake ya kuwania ugavana wa Nairobi dhidi ya Sakaja katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *