#Local News

GACHAGUA ADAI WAGENI NA WAFU WANASAJILIWA KUPIGA KURA 2027

Kiongozi wa chama cha DCP Rigathi Gachagua ameishutumu serikali ya Rais William Ruto kwa madai ya kupanga kuvuruga uchaguzi wa mwaka ujao kupitia usajili wa raia kutoka Uganda pamoja na Wakenya waliofariki.

Akizungumza nchini Marekani katika mkutano na Wakenya wanaoishi ughaibuni, Gachagua amedai hatua hiyo inalenga kumsaidia Rais Ruto kubaki madarakani, huku akisema umaarufu wa rais unaendelea kupungua.

Madai hayo yanajiri wakati mjadala kuhusu usajili wa wapiga kura ukizidi kushika kasi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027, huku serikali ikipinga madai ya usajili wa wageni.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *