#uncategorized

MAN UNITED TAABANI BAADA YA KUDHALILISHWA 4-1 NA COMO

Manchester United inakabiliwa na presha zaidi baada ya ripoti kudai kuwa mshambuliaji Matheus Cunha alizozana na kocha Michael Carrick wakati wa kichapo cha mabao manne kwa moja dhidi ya Como katika Ligi ya Mabingwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Samuel Luckhurst wa gazeti la The Sun, wawili hao walikuwa na mazungumzo makali nje ya kamera, huku nahodha Bruno Fernandes pia akiripotiwa kutoridhishwa na maamuzi ya mbinu za kocha.

Cunha alitolewa wakati wa mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na Amad Diallo, huku matokeo hayo yakizidisha maswali kuhusu uhusiano kati ya Carrick na wachezaji wake.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *