UPINZANI WAMJIBU RUTO KWA KUMKOSOA UHURU
Viongozi wa upinzani wamemjibu Rais William Ruto kufuatia matamshi yake ya hivi karibuni dhidi ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, wakimkosoa kwa kile wanachodai ni kushindwa kuboresha maisha ya Wakenya.
Wakiongozwa na Kiongozi wa Chama cha People’s Party of Kenya Ndindi Nyoro na Kiongozi wa Jubilee Fred Matiang’i, viongozi hao wamemtuhumu Ruto kumtumia Uhuru kama kisingizio cha changamoto zinazokabili serikali yake.
Viongozi hao waliokuwa katika ziara ya Kaunti ya Narok pia wameahidi kuunganisha upinzani na kumsimamisha mgombea mmoja wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































