MVULANA WA MIAKA 17 AUAWA MATUNGU
Polisi katika eneo la Matungu, kaunti ya Kakamega, wanachunguza mauaji ya mvulana wa miaka 17, Paul Wanjala, ambaye mwili wake ulipatikana katika shamba la miwa Oktoba 10, akiwa na shoka lililokwama upande wa kulia wa kichwa chake.
Mama wa marehemu amewaambia polisi kuwa mwanawe alikula chakula cha jioni na rafiki yake kabla ya kuondoka kwenda kulala, lakini aliarifiwa asubuhi iliyofuata kuwa mvulana huyo amepatikana amefariki.
Wapelelezi walikusanya ushahidi katika eneo la tukio na kuondoa shoka hilo kwa uchunguzi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































