#Local News

RUTO ATETEA REKODI YAKE YA UONGOZI

Rais William Ruto ametumia maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Mashujaa kutetea utendakazi wa serikali yake, akisisitiza kuwa imetekeleza ahadi zilizotolewa kwa Wakenya wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2022.

Ruto ametaja hatua zilizopigwa katika uchumi, elimu, afya, kilimo na miundombinu kama baadhi ya mafanikio ya utawala wake, akisema serikali inaendelea kutekeleza ajenda yake ya maendeleo.

Ruto anashikilia kuwa juhudi za serikali yake zinalenga kuimarisha maisha ya Wakenya na kutimiza ahadi ilizotoa kwa wananchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *