KENYA YASHEHEREKEA SIKU YA MASHUJAA
Sherehe za Siku ya Mashujaa 2026 zimevutia maelfu ya Wakenya katika uwanja wa Kipchoge Keino mjini Eldoret, huku muziki, ngoma na gwaride la kijeshi vikitarajiwa kuongoza hafla hiyo.
Umati wa wananchi ulianza kuwasili uwanjani humo kuanzia saa kumi alfajiri, wakijitokeza kuwaenzi mashujaa wa taifa
Maadhimisho ya mwaka huu yanaandaliwa kwa pamoja na kaunti za Uasin Gishu, Nandi na Elgeyo-Marakwet, huku Eldoret ikiwa mwenyeji wa hafla hiyo ya kitaifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































