KENYA POLICE YATENGANA NA MUYOTI NA BARAZA
Kenya Police FC imetengana na kocha mkuu Nicholas Muyoti na msaidizi wake John Baraza baada ya mechi mbili pekee za ligi kuu ya FKF msimu wa 2026/27.
Klabu hiyo imesema wawili hao wameondoka ili kuendeleza masomo yao na kupata leseni ya ukocha ya CAF-A, baada ya Kenya Police kuanza msimu kwa sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Migori Youth na kichapo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya AFC Leopards.
Katika taarifa yake, klabu hiyo imesema Muyoti na Baraza walijiunga kwa makubaliano kuwa wangeachiliwa pindi fursa ya kuimarisha sifa zao za ukocha itakapojitokeza.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































