RUTO ASEMA UJENZI WA HOSPITALI YA KITALE UTAENDELEA
Rais William Ruto ameapa kuwa uboreshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kitale utaendelea bila kukatizwa, huku mvutano wake na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya ukiendelea.
Akizungumza Kapsabet, kaunti ya Nandi, Ruto ametetea rekodi ya serikali yake na kuendelea kukosoa Upinzani, akidai hauna mwelekeo wala maono ya kuwaongoza Wakenya.
Ruto amewataka wakenya kuwaombea viongozi wa upinzani, akiwashutumu kwa kukosa dira ya kitaifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































