#Local News

MATIANG’I AITAKA SERIKALI KUWEKA WAZI MKATABA WA DANGOTE LAMU

Kiongozi wa Chama cha Jubilee Fred Matiang’i ameongeza shinikizo kwa serikali kufichua maelezo ya mradi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote wenye thamani ya shilingi trilioni 2.2 Lamu.

Matiang’i pia ametaka serikali kuweka wazi makubaliano kuhusu haki za uchimbaji madini yaliyo katika mkataba huo, akisema hatua hiyo ni muhimu kwa uwazi na uwajibikaji.

Kauli yake inaendeleza wito kutoka upande wa upinzani wa kutaka maelezo zaidi kuhusu mradi huo mkubwa wa uwekezaji na masharti yaliyokubaliwa kati ya serikali na Dangote.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *