OWINO APEWA NAFASI KIKOSI CHA KENYA SEVENS MAURITIUS
Mchezaji wa Menengai Oilers Glacious Owino ameitwa katika kikosi cha Kenya Sevens kitakachoshiriki Mashindano ya Kombe la Afrika ya Raga ya Wachezaji Saba nchini Mauritius wikiendi hii.
Owino ameungana na washambuliaji wa Kabras Patrick Sabatia na Brian Mutua, Dennis Livoi wa Mwamba pamoja na Lucky Onyango wa Oilers, huku kocha Kevin Wambua akichanganya vipaji chipukizi na wachezaji wenye uzoefu.
Owino alitawazwa mchezaji bora wa Christie Sevens wiki mbili zilizopita na kuonyesha kiwango thabiti katika hatua zote tano za mzunguko wa kitaifa, huku kasi na maamuzi yake yakimpa nafasi ya kuwania taji la Afrika ambalo Kenya haijashinda kwa misimu miwili.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































