BEI ZA VYAKULA KUTARAJIWA KUPANDA KENYA
Wakenya wanatarajiwa kukabiliwa na ongezeko zaidi la bei za vyakula katika wiki zijazo kutokana na kupanda kwa gharama ya mafuta, uzalishaji na ukame unaotishia upatikanaji wa bidhaa.
Utafiti wa Benki Kuu ya Kenya wa Septemba 2026 unaonyesha kuwa maziwa, unga wa mahindi, bidhaa za ngano, sukari na mboga huenda zikapanda bei, huku asilimia 64 ya wakul.ima na wafanyabiashara waliohojiwa wakitarajia mfumuko wa bei kuongezeka katika mwezi ujao.
Hata hivyo, asilimia 61 wanatarajia hali kutengamaa katika miezi mitatu ijayo, wakitumai kuwa mvua za Oktoba hadi Desemba zitaboresha mavuno na kuongeza upatikanaji wa chakula sokoni.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































