#Local News

SAKAJA AONYA SHULE NAIROBI ZINAWEZA KUFUNGWA KWA SABABU YA EL NINO

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ameonya kuwa baadhi ya shule katika kaunti hiyo huenda zikafungwa iwapo mvua kubwa ya El Nino inayotarajiwa katika kipindi cha wiki mbili itahatarisha usalama wa wanafunzi.

Sakaja amesema Kaunti ya Nairobi imeimarisha maandalizi ya kukabiliana na mvua hizo na uwezekano wa mafuriko, huku maafisa wakipitia mikakati ya kulinda wakazi na miundombinu muhimu.

Gavana huyo amesema mawasiliano yatakuwa muhimu katika kuwafahamisha kwa wakati wakazi wa maeneo yaliyo hatarini kuhusu tahadhari na hatua za usalama wakati wa mvua hizo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *