#Football #Sports

PSG YAICHAPA BARCELONA MABAO 4-2

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Paris Saint-Germain, wameilaza Barcelona mabao manne kwa mawili katika mechi kali iliyochezwa mjini Paris, na kuendeleza ushindi wao katika mashindano hayo.

Vitinha alivunja sare ya mabao 2-2 dakika ya 81 kwa shuti kali nje ya eneo la hatari, kabla ya Fabian Ruiz kufunga bao la nne na kuipa PSG ushindi wa tatu mfululizo katika mashindano ya msimu huu.

Desire Doue na Lucas Hernandez walifunga mabao mengine ya PSG, huku Xavi Espart na Lamine Yamal wakiifungia Barcelona, ambayo ilikaribia kuondoka na sare kabla ya mabingwa hao kutawala dakika za mwisho.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *