RUTO AWASHAMBULIA VIONGOZI WA UPINZANI
Rais William Ruto ameendeleza ukosoaji wake dhidi ya viongozi wa upinzani, akiwatuhumu kwa kutafuta mamlaka bila kuwajibika, kuchochea ukabila na chuki, na kukosa mipango mbadala ya kukabili changamoto za taifa.
Rais amewataja viongozi wa upinzani kama wafanyabiashara wa hasira na mitazamo hasi, akisema wanategemea upinzani dhidi ya serikali yake badala ya kutoa suluhisho la matatizo yanayowakabili Wakenya.
Miongoni mwa viongozi aliowakosoa ni Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































