JENGO LA GHOROFA NYINGI LILILOKUWA LIKIJENGWA LIMEPOROMOKA EASTLEIGH NAIROBI

Jengo la ghorofa nyingi lililokuwa likijengwa limeporomoka katika barabara ya 9, eneo la Eastleigh jijini Nairobi, huku kukiwa na hofu kuwa watu kadhaa huenda wamenasa chini ya vifusi. Idadi ya watu walioathiriwa na tukio hilo bado haijabainika, huku shughuli za uokoaji zikitarajiwa kubaini iwapo kuna watu walionasa kwenye vifusi vya jengo hilo. Walioshuhudia wamesema hali […]

WAZIRI DUALE AMEAHIDI KUKABILIANA NA UFISADI UNAOHUSIANA NA FEDHA ZA EBOLA

Waziri wa Afya Aden Duale ameahidi kuchukua hatua za kuziba mianya yote ya ufisadi katika matumizi ya fedha zilizotengwa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini. Amesema wizara yake itaimarisha usimamizi wa fedha hizo ili kuhakikisha zinatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa, yakiwemo kuzuia maambukizi na kuimarisha huduma za afya. Duale amesema hatua hizo zinalenga kuzuia kujirudia kwa […]

EPL: CHELSEA vs TOTTENHAM

Ligi Kuu ya Uingereza  inaendelea leo usiku kwa mechi kati ya Ipswich Town na Nottingham Forest itakayochezwa saa nne usiku. Kesho, Aston Villa itamenyana na Manchester City saa nane unusu, huku Coventry ikikabiliana na Fulham na Arsenal ikiikaribisha Everton saa kumi na moja jioni, kabla ya Chelsea kukutana na Tottenham saa moja unusu usiku. Jumapili, […]

KAZI ZA MWISHO ZA TALANTA STADIUM ZAKAGULIWA

Kazi za mwisho na marekebisho katika uwanja wa Talanta Stadium zimekaguliwa huku Kenya ikiimarisha maandalizi ya kuandaa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027. Katibu Mkuu katika Wizara ya Ulinzi Patrick Mariru aliongoza kikao cha tathmini uwanjani Alhamisi akishirikiana na mwenzake wa Michezo Elijah Mwangi pamoja na maafisa wa Sports Kenya na Jeshi […]

KENYA NA AFRIKA KUSINI KUKUTANA KATIKA SPORTPESA LEGENDS CUP

Kenya Rugby Legends itaandika historia mwaka 2027 itakapokutana na South Africa Rugby Legends katika mfululizo wa mechi mbili za SportPesa Legends Cup, mashindano yatakayopanuka nje ya Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza. Mechi ya kwanza itachezwa Nairobi Mei 8, 2027, kabla ya kikosi cha Kenya kusafiri hadi Cape Town kwa mechi ya marudiano Julai 4. […]

KANJA AONYA POLISI WANAOWANYANYASA UMMA

Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja amewaonya maafisa wanaohusika na utovu wa nidhamu kuwa watawajibika kwa matendo yao, kufuatia kushambuliwa kwa mwandishi wa habari jijini Nairobi alipokuwa akiripoti maandamano dhidi ya gharama ya juu ya mafuta. Kanja amesema tukio hilo lililonaswa na kamera na kurushwa na vyombo vya habari limeichafua taswira ya Huduma ya Kitaifa […]

MBADI ATUPILIA MBALI MADAI YA NYORO KUHUSU KPC

Waziri wa Hazina ya Kitaifa John Mbadi amepuuzilia mbali madai ya kiongozi wa People’s Party of Kenya, Ndindi Nyoro, kuwa Rais William Ruto anapanga kutwaa kampuni ya Kenya Pipeline kupitia bilionea wa Nigeria Aliko Dangote. Mbadi amesema uuzaji wa asilimia 25 ya hisa za kampuni hiyo ulikuwa shughuli halali ya kibiashara kati ya muuzaji aliyejitolea […]

NYORO AIBUA MASWALI KUHUSU HISA ZA KENYA PIPELINE

Mbunge wa Kiharu na kiongozi wa People’s Party of Kenya, Ndindi Nyoro, amedai kuwa ununuzi wa takriban robo ya hisa za kampuni ya Kenya Pipeline ni mwanzo wa mpango wa bilionea wa Nigeria Aliko Dangote na Rais William Ruto kutwaa udhibiti wa kampuni hiyo ya umma. Nyoro pia amemshutumu Rais Ruto kwa kuingilia mchakato wa […]

BUNGE LATAKA SERIKALI KUMALIZA MGOMO WA WAHADHIRI

Bunge la Kitaifa limetoa wito kwa serikali kuingilia kati haraka na kumaliza mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma unaoendelea kuvuruga masomo. Akifika mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Umma, Katibu Mkuu katika Wizara ya Elimu anayesimamia elimu ya juu, Beatrice Inyangala, amesema wizara inaendelea kufanya mazungumzo na wadau kutafuta suluhu ya […]

ATWOLI APINGA AZMA YA SIFUNA KUWANIA URAIS

Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli, amepinga azma ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuwania urais, akisema bado hajajiandaa kuongoza nchi Akizungumza katika mazishi eneo la Kanduyi, kaunti ya Bungoma, Atwoli ametangaza kumuunga mkono Rais William Ruto kuchaguliwa tena mwaka 2027, huku akionya Jamii ya Waluhya dhidi ya kutumiwa kisiasa na viongozi vijana Atwoli pia […]