RUTO ATAKA UPINZANI KUTOA SULUHISHO MBADALA
Rais William Ruto amewataka wapinzani wake kuwasilisha sera mbadala na suluhisho badala ya kukosoa serikali yake bila kupendekeza hatua zinazoweza kutekelezwa.
Ruto amesema viongozi wanapaswa kuelekeza nguvu zao katika mawazo na mipango ya maendeleo badala ya siasa za kikabila na mashambulizi binafsi, akisisitiza kuwa serikali yake iko tayari kukosolewa na kuchunguzwa.
Rais huyo pia ametetea kauli mbiu yake ya “Usawa ni Sawa”, akisema serikali yake inasambaza miradi ya maendeleo nchini kote bila ubaguzi, tofauti na tawala zilizotangulia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































