UPINZANI WAPINGA AHADI ZA RUTO ZA KUPUNGUZA KODI
Viongozi wa upinzani wamepuuza ahadi za Rais William Ruto za kupunguza kodi kwa Wakenya wanaopata chini ya shilingi elfu 32,333, wakizitaja kuwa mbinu za kampeni.
Wakizungumza katika kaunti ya Narok, Viongozi hao Martha Karua, Fred Matiang’i na Ndindi Nyoro wametilia shaka rekodi ya serikali katika kutekeleza ahadi zake.
Viongozi hao wamesema juhudi za kuunda muungano imara wa upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027 zinaendelea kushika kasi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































